DK CHENI APATA AJALI YA GARI | BONGOJAMII

DK CHENI APATA AJALI YA GARI

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Dk Cheni
MWIGIZAJI wa kitambo Bongo, Mahsein Awadh ‘Dk Cheni’ amenusa kifo baada ya kupata ajali mbaya baada ya gari lake kupasuka tairi la mbele na kuparamia nguzo kisha kupata maumivu makali kwenye bega la mkono wa kushoto.

Kwa mujibu wa shuhuda wetu, Cheni alikumbwa na mkasa huo usiku wa Alhamisi iliyopita maeneo ya Bamaga-Mwenge, Dar, wakati akitokea Tegeta kwenye sherehe ya mmoja wa jamaa zake ambapo alipofika eneo hilo, ghafla tairi la upande wa kulia lilipasuka na kukosa mwelekeo kisha kuivaa nguzo iliyopo pembeni kabla ya kukwama kwenye jiwe kubwa.

Ijumaa Wikienda lilipomtafuta Dk Cheni alifunguka: “Dah! Ni kweli nilipofika pale Bamaga, ghafla nilisikia gari limekuwa zito na hapohapo tairi la mbele likapasuka. Gari lilikosa mwelekeo nikalielekeza kwenye nguzo, ninamshukuru Mungu sikupata jeraha kubwa, nimeumia bega la kushoto ila ninaendelea vizuri,” alisema Dk Cheni.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts