Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafaya Kibiti.Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha makasha ya risasi(magazine) ambazo ni miongoni mwa makasha 8 yaliyokuwa ya kitumiwa na wahalifu katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) MussaAlli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi,Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. Katikat ukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13 ambao walikuwa wakifanya mauaji Kibiti.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akielezea baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 walioua wakatika eneo la Tangi bovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti ambapo jumla ya silaha 8 ainaya SMG, risasi 158,pikipiki 2, pamoja na begi la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha silaha aina ya SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8 zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu 13 walioua wakatika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo laTangi bovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti.Wa kwanza kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi,Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas.–
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiongea na wananchi wa Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka kukagua eneo la tukio walipouawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangi bovu. –
Picha na Jeshi La Polis
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka