UHURU KENYATA AIBUKA MSHINDI WA KITI CHA URAIS NCHINI KENYA | BONGOJAMII

UHURU KENYATA AIBUKA MSHINDI WA KITI CHA URAIS NCHINI KENYA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Tume ya taifa ya uchaguzi Kenya imemtangaza Rais Uhuru Kenyatta wa chama cha Jubilee kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Jumanne.

Rais Kenyatta alipata kura 8, 203, 290.. ambayo ni asilimia 54 naye mpinzani wake mkuu, mgombea wa muungano wa upinzani wa National Super Alliance Raila Odinga akapata kura milioni 6,762,224 ambayo ni asilimia 44.

Akitangaza matokeo hayo mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Kenya IEBC Wafula Chebukati alisema kuwa ni asilimia 78 ya wapiga kura milioni 19 waliosajiliwa pekee walioshiriki katika shuguhuli hiyo ya kidemokrasia.

Alisema kuwa licha ya matatizo machache kukumba mfumo mpya wa kutangazia matokeo, tume yake ilifanikiwa kutangaza matokeo hayo bila tashwishi yoyote.


Aliongezea kuwa hatua zilizochukuliwa kuandaa uchaguzi huo ni hakikisho tosha la ukomavu wa kidemokrasia nchini.

Alisema kuwa Wakenya wengi walijitokeza na kivumilia hali ya anga ili kushiriki katika zoezi hilo la kidemokrasia kutokana na uaminifu walio nao kwa tume hiyo ya uchaguzi.

Aliongezea kwamba licha ya kukumbwa na changamoto chungu nzima katika mahakama waliweza kuandaa uchaguzi huo kwa njia ya haki uwazi na uhuru,

Akitoa hotuba yake rais Uhuru Kenyatta amewashukuru wafuasi wake na Wakenya wote kwa jumla kwa kumpatia muhula mwengine.

Aidha amemtaka mpinzani wake mkuu Raila Odinga na wafuasi wake kushirikiana naye katika kujenga Kenya akisema kuwa Uchaguzi huja na kumalizika lakini wakenya ni sharti wasalie kama mandugu na majirani wema.

''Katika kila mashindano kuna mshindi na aliyeshindwa ,hivyobasi namuomba ndugu yangu mkubwa Raila Odinga na wafuasi wake kushirikiana nami katika kulijenga taifa hili kwa sababu uchaguzi huja na kumalizika lakini wakenya ni sharti wanedlea kuwa majirani wema'', alisema Uhuru Kenyatta.

Na muda mfupi tu baada ya Uhuru Kenyatta kutanzwa rais mteule wafuasi wake kote nchini walisherehekea ushindi huo kwa vifijo na nderemo.

Muungano wa upinzani ulikuwa umepinga utaratibu uliokuwa unatumiwa na tume hiyo kupeperusha matokeo ya uchaguzi huo.

Aidha, viongozi wa muungano huo walikuwa wamedai mitambo ya tume hiyo ilidukuliwa na matokeo kubadilishwa.


Viongozi hao walikuwa Alhamisi wametangaza kwamba mgombea wao, Bw Odinga ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu katika serikali ya Mwai Kibaki, kuwa mshindi wa uchaguzi huo.
Matoeko kamili ya wagombea wote kama yalivyotangazwa na Bw Chebukati

Mgombea Chama Kura Asilimia
Uhuru Kenyatta Jubilee 8,203,290 54.27
Raila Odinga ODM 6,762,224 44.74
Mohamed Abduba Dida ARK 38,093 0.25
Japheth Kavinga Kaluyu Mgombea wa kujitegemea 16,482 0.08
Michael Wainaina Mwaura Mgombea wa kujitegemea 13,257 0.09
Joseph Nthiga Nyagah Mgombea wa kujitegemea 42,259 0.28
John Ekuru Aukot Thirdway Alliance 27,311 0.18
Cyrus Jirongo UDP 11,705 0.08

Muda mfupi kabla ya matokeo hayo kutangazwa, Muungano wa upinzani ulikuwa umesema hauungi mkono tangazo la matokeo la IEBC.

Ajenti mkuu wa muungano huo Musalia Mudavadi alisema malalamiko yaliyowasilishwa na muungano huo kwa tume hayajashughulikiwa ipasavyo.

Bw Mudavadi amesema baada ya kukutana na tume hiyo, walifahamishwa kwamba baadhi ya mambo yao yatashughulikiwa baada ya matokeo kutangazwa.

"Mikutano ilikuwa kama shughuli ya uhusiano mwema tu," amesema.
Tume ilikuwa imewaalika maajenti wakuu kwa mkutano kabla ya kutoa tangazo la matokeo.
Lakini upinzani umesema hautashiriki katika kukubaliana na tangazo la tume hiyo.

Naibu ajenti wa muungano huo James Orengo ametilia shaka waangilizi ambao walikuwa wamesema uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.

Amesema waangalizi hao walifaa kuchunguzwa kwanza, Bw Orengo amesema pia kwamba muungano huo haupangi kwenda kortini kupinga matokeo.

Viongozi wa kanda ya Afrika Mashariki, wakiwemo Rais wa Rwanda Paul Kagame na Yoweri Museveni wa Uganda wamempongeza Rais Kenyatta kwa ushindi wake.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts