Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza kukamata watu wapatao 150 kuanzia Agosti 14 hadi 17 mwaka huu, kwa makosa ya kuwabughuzi abiria katika maeneo mbalimbali ya jiji katika vituo vya mabasi.
Wakati akizungumza na wanahabari jana jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamanda Lucas Mkondya, alisema watuhumiwa hao walikamatwa kufuatia misako na operesheni kali iliyofanywa na polisi, na kwamba watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili.
“Stendi ya mabasi ya Ubungo walikamatwa 39, Posta 12, Ferry 7, Tegeta 12, Tandika 16, Mnazimmoja 6, Stesheni 5, Manzese 12, Bunju 8 na Stereo 7,” amesema.
Katika hatua nyingine, Kamanda Mkondya alisema Jeshi la Polisi katika nyakati tofauti ilikamata watuhumiwa 167 kwa makossa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya, unyang’anyi wa kutumia sialaha na utapeli, kucheza kamali na kuuza pombe haramu ya gongo.
“Katika operesheni hii kali ambayo ni endelevu, jumla ya kete 96 za dawa ya kulevya, misokoto ya bangi 107, gongo lita 60 zilikamatwa. Tunaomba raia wema kuendelea kutoa taarifa za wahalifu ili tuwakamate na hatua kali za kisheria zifuatwe dhidi yao,” alisema.
Alisema watuhumiwa wote wanaendelea kuhojiwa kulingana na makossa yao na kwamba upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria zaidi.
Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka