TANZIA: ALIYEWAHI KUWA MKUU WA WILAYA HANDENI AFARIKI DUNIA | BONGOJAMII

TANZIA: ALIYEWAHI KUWA MKUU WA WILAYA HANDENI AFARIKI DUNIA

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD
Dar es Salaam. Aliyewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni (2012) na nguli wa habari nchini, Rweyemamu Muhingo(67) amefariki leo katika hospitali ya Aga Khan jijini.

Muhingo ameacha simanzi katika tasnia ya habari, familia na taifa kwa ujumla.

Muhingo ambaye awali alibahatika kuteuliwa na Rais wa Awamu ya nne, Jakaya Kikwete kuongoza wakazi wa Halmashauri ya Handeni kabla ya kuhamishiwa Makete na baadaye Morogoro mjini.

Kabla ya uteuzi huo, aliwahi kuwa mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi linalochapisha magazeti ya Mwanaspoti na The Citizen. Pia aliwahi kuandikia gazeti la Mtanzania

Mtoto wa marehemu, Mwesigwa Muhingo ameliambia gazeti hili leo kwamba, amefariki kwa maradhi ya Myelofibrosis, yanayotokana na mifupa kushindwa kutengeneza damu.

“Alhamisi tulikuwa na mpango wa kumsafirisha nje ya nchi ingawa tulikuwa hatujapata hospitali hali yake ilibadilika ghafla leo saa 3:00 Mungu akamchukua’’amesema Muhingo.

Mwananchi:

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts