WALIONASWA NA MZIGO WA ALMASI WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO | BONGOJAMII

WALIONASWA NA MZIGO WA ALMASI WAPANDISHWA KIZIMBANI LEO

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka
BONYEZA HAPA KU-DOWNLOAD

Baada ya Serikali kuanza kuwashughulikia wale wote wanaohujumu uchumi wa nchi na kuiibia nchi rasilimali zake, watuhumiwa waliokamatwa na mzigo wa Almasi zenye thamani ya shilingi bilioni 32.3 katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), wamefikishwa katika Mahakama ya Kisutu leo asubuhi Septemba 15.


Mzigo huo wa Almasi uliokuwa unatoka mgodi wa Mwadui ulizuiliwa na Serikali kwa lengo la kuufanyia tathmini upya ili kujua thamani halisi baada ya thamani iliyokuwa imetajwa awali kutiliwa mashaka na Serikali.


Baada ya kubainika kuwa wahusika walidanganya thamani, Jeshi la Polisi liliwashikilia watuhumiwa wanne huku uchunguzi na hatua nyingine za kisheria zikifuatwa baada ya kuzuiwa kwa mzigo huo.


Mgodi wa Mwadui unamilikiwa kwa ubia kati ya Serikali na Kampuni ya Petra Diamonds ya Afrika Kusini ambapo Serikali ina hisa 25% na Petra Diamonds ina hisa 75%.

Bonyeza HAPA kudownload applicationi ya Bongojamii Blog kwenye simu yako ili kupata habari zetu Haraka

Featured Posts